Friday, August 3, 2018

KAMPUNI YA PETROBENA WASAMBAZAJI WA PEMBEJEO NCHINI WAANZA KUTEKELEZA KWA VITENDO AGIZO LA RAIS MAGUFULI.


MKURUGENZI MTENDAJI WA KAMPUNI YA PETROBENA EAST AFRICA LIMITED PETER KUMALILWA MWENYE KIPAZA SAUTI ALIYESIMAMA AKIELEZEA MIPANGO YA KAMPUNI HIYO KATIKA KUMKWAMUA MKULIMA WA TANZANIA.

MOROGORO

Na William Bundala.
KAMPUNI ya usambazaji ya Pembejeo ya PETROBENA EAST AFRICA LTD imeanza kuunga mkono kwa vitendo Juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungwano wa Tanzania Mh John Pombe Magufuli kwa kuhakikisha wanafikisha pembejeo za kilimo kwa wakati  kwa wakulima nchini.

Akiongea mkoani Morogoro katika mafunzo ya matumizi sahihi ya pembejeo za kilimo kwa maafisa kilimo na wasambazaji wa pembejeo,Mkurugenzi wa Kampuni ya PETROBENA Peter Kumalilwa amesema kuwa wameamua kuweka Ghala kubwa mkaoni Morogoro ili kuhakikisha wakulima wa mkoa huo na mikoa jirani wanapata pembejeo kwa haraka kupitia wauzaji wadogo na wakubwa.

Kumalilwa amesema kuwa PETROBENA ikiwa wakala mkuu wa kampuni ya Mbolea ya  YARA watahakikisha mbolea inapatikana katika katika kipindi chote na siyo kama ilivyo sasa katika maeneo mengi ambapo mbolea inaanza kupelekwa wakati wa msimu hali inayosababisha kuchelewa kutokana na ubovu wa miundo mbinu pamoja na umbali wa walipo wahitaji.

Sambamba na hayo amongeza kuwa katika mkoa wa Morogoro wanatarajia kuwa na wauzaji wa pembejeo wapatao mia saba (700) katika wilaya zote Sita ambao  watapewa mafunzo ya matumizi bora ya pembejeo itakayowasaidia kuwapa elimu wakulima wa mazao mbali mbali mkoani humo wakiwemo wa Miwa,Mpunga,Mahindi,Mboga mboga na mazao mengine.

Awali akiongea katika mafunzo hayo Afisa Biashara wa kampuni ya YARA nyanda za juu kusini John Meshak amesema kuwa wameamua kuzindua ghala la mbolea Morogoro kwa kuwa kuna wakulima wengi wanaolima mazao mengi ila hawapati nafasi ya kupata mbolea bora na kwa wakati hali inayopunguza kasi ya uzalishaji wa mazao yao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wakulima wa Miwa wilaya ya Kilombero Bakari Mkangamo akiongea kwaniaba ya wakulima wenzake ameipongeza kampuni ya PETROBENA ambao ni wakala mkuu wa YARA kwa kuwafikishia pembeo kwa wakati,na kuongeza kuwa kuanzia msimu ujao uzalishaji utaongezeka kwa kuwa wakulima wamelima na kuwekea mbolea kwa wakati tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Mwishoni mwa mwaka jana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh John Pombe Magufuli alitoa wito kuhakikisha kwamba Mbolea na pembejeo zingine zinapatikana muda wote zinapohitajika tena na kwa gharama nafuu ambapo Kampuni ya PETROBENA EAST AFRICA LTD ambao ni wakala  wakuu wa Kampuni ya Mbolea ya YARA wameanza kutekeleza agizo hilo kwa mikoa ya Dar es salaam,Tabora,Morogoro,Njombe na Arusha.


MATUKIO KATIKA PICHA:
MTAALAMU WA KILIMO KUTOKA KAMPUNI YA YARA MAULID MKIMA AKITOA DARASA LA KWA MAAFISA KILIMO NA MAAFISA WA PEMBEJEO KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO WA OFISI MPYA YA PETROBENA MKOANI MOROGORO.

AFISA BIASHARA WA KAMPUNI YA YARA NYANDA ZA JUU KUSINI JOHN MESHACK AKIONGEA NA MAAFISA KILIMO PAMOJA NA WAUZAJI WA PEMBEJEO SABABU ILIYOWAFANYA WAWEKE GHALA LA PEMBEJEO MKOANI MOROGORO.

 MKURUGENZI WA KAMPUNI YA PETROBENA EAST AFRICA LIMITED PETER KUMALILWA MWENYE T-SHIRT NYEUPE AKISIKILIZA KWA MAKINI DARASA LILILOKUWA LIKITOLEWA NA MTAALAMU WA KILIMO KUTOKA KAMPUNI YA YARA BWANA MAULID MTIMA HAYUPO PICHANI.

 MAAFISA KILIMO NA WAUZAJI WA PEMBEJEO KUTOKA WILAYA ZA MKOA WA MOROGORO WAKIWA MAKINI DARASANI KATIKA MAFUNZO YA MATUMIZI BORA YA PEMBEJEO NA UMUHIMU WA KUTUMIA MBOLEA

 MKURUGENZI WA UTAWALA NA FEDHA KUTOKA KAMPUNI YA PETROBENA SABENA KUBINI ALIYESIMAMA KULIA AMEVAA T-SHIRT NYEUPE PAMOJA NA MAAFISA WENGINE WA PETROBENA NA YARA WAKIWA DARASANI KUSIKILIZA ELIMU YA MATUMIZI BORA YA MBOLEA KUTOKA KWA MTAALAMU WA KILIMO WA KAMPUNI YA YARA HAYUPO PICHANI.


 MAAFISA KILIMO NA WAUZAJI WA PEMBEJEO WAKIWA MAKINI KUSIKILIZA MAFUNZO KUHUSU UMUHIMU WA MATUMIZI BORA YA MBOLEA NA MADHARA YA KUTUMIA MBOLEA TOFAUTI NA MAELEKEZO YA WATAALAMU.

 MAAFISA KILIMO,WAUZAJI WA PEMBEJEO NA WAFANYAKAZI WA KAMPUNI YA PETROBENA WAKIWA DARASANI WAKIENDELEA KUPATA MAFUNZO YA MATUMIZI BORA YA MBOLEA KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO WA OFISI MPYA ZA PETROBENA ZILIZOPO NANE NANE MKOANI MOROGORO.

 MAFUNZO YAKIENDELEA KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO WA PETROBENA MKOANI MOROGORO

No comments:

Post a Comment