WAZIRI wa
Nchi OR-TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo amekutana na Waziri wa Ujenzi,
Mawasiliano na Uchukuzi Pro. Makame Mbarawa na Naibu Waziri wa Ardhi Mhe.
Angelina Mabula kujadili mustakabali wa mgogoro wa Ardhi uliopo kati ya
wananchi wanaonzunguka eneo la uwanja wa Ndege wa Kia na mwendeshaji wa Uwanja
huo Kampuni ya KADCO.
Mgogoro huo unaohusisha zaidi ya kaya 1200 zilizopo katika Mikoa
ya Kilimanjaro na Arusha zinatakiwa kupisha upanuzi wa uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa Kilimanjaro.
Kaya hizo ambazo zipo katika vijiji vilivyopimwa Kisheria lakini
maeneo ya vijiji hivyo yanaingiliana na eneo la uwanja wa KIA na hivyo
kusabisha mgogoro baina ya Menejimentinya Uwanja na wananchi hao.
Hali hiyo ilipelekea kuundwa kwa timu ya Ufuatiliaji na
utafutaji wa suluhu ya mgogoro huo ambayo inaundwa na wizara tatu za Tamisemi,
Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi, Wizara ya ardhi wakuu wa Mikoa miwili ya
Kilimanjaro na Arusha pamoja na wataalamu kutoka katika sekta mbalimbali za
ardhi na mawasiliano ya anga.
Kupitia kikao hicho kiliziamia kuwa vijiji hivyo vifanyiwe
uthamini upya ili wananchi wa maeneo hayo waweze kulipwa Fidia na kuachia
maeneo hayo kwa ajili ya upanuzi wa kiwanja cha ndege.
Kwa
Pamoja viongozi hao wamekubaliana kuanza mchakato wa kufuta hati za vijiji
hivyo na kuanza mchakato wa kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa eneo hilo
kwa maslahi mapana ya Taifa.
Mgogoro
kati ya wananchi wanaozunguka uwanja wa ndege wa KIA na kampuni ya KADCO
umekuwako toka mwaka 1998 na umesababisha misuguano na hisia kali kwa muda
mrefu hali iliyosababisha Serikali kuamua kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa
mgogoro huu.
No comments:
Post a Comment