Jaji Mkuu Prof. Juma
-ARUSHA
JAJI
Mkuu wa Tanzania Professa Ibrahimu Juma amewataka Watendaji na Wataalamu wa
Mahakama, kuacha kuficha upungufu na makosa waliyonayo kwani Benki ya Dunia
(WB), huangalia wananchi wa kawaida, wafanyabiashara na wanyonge katika jamii.
Kauli
hiyo aliitoa jana mjini hapa kwenye Kikao kazi cha kutathimini changamoto
ambazo WB ilizibaini na kuzitaja kuwa msukumo ulioifanya ikubali kushirikiana
na Serikali ya Tanzania katika mradi wa kuifadhili Mahakama ya Tanzania.
Watendaji
na wataalamu wa Mahakama wapo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha
Arusha (AICC), tangu Machi 5 hadi Machi 15, mwaka huu wakitathimini utekelezaji
wa mpango mkakati wa miaka mitano 2015-2020 na utekelezaji wa mradi wa
maboresho ya utoaji huduma za mahakama.
Katika
mkutano huo, Jaji Mkuu Prof. Juma aliwataka watendaji na wataalamu hao
kuhakikisha wanafanya tathimini ya wazi kuhusu makosa na upungufu waliofanya
kwa miaka miwili na nusu ya uhai wa Mpango mkakati wa 2015/16 na 2019 mpaka
2020.
“Tusipokubali
makosa hatutapata nafasi ya kujirekebisha na tutarudia makosa hay ohayo wakati
wabia wetu Benki ya Dunia na Serikali wanatutathimini pia.
“Hapa
ni lazima tutambue WB lazima itafanya tathimini yake kama mbia. Hapana shaka,
itarejea itatathimini kwa kiasi gani zile changamoto zilizozitaja katika andiko
lake la mradi zinatekelezwa,” alisema Jaji Mkuu Prof. Juma na kuongeza:
“Baadhi
yake zinakugusa upatikanaji taarifa kwa wananchi, zinaweza kuchukuliwa kuwa
suala dogo. Lakini, kwa mwananchi wa kawaida upatikanaji wa taarifa ni nyenzo
muhimu katika kumuwezesha kupata haki yake mahakamani,”alisema.
Aliyataja
maandiko yaliyo kwenye mradi kuwa WB iligusia wananchi na wafanyabiashara ambao
hukosa taarifa za kimahakama kuwaongoza kufungua mashauri, ada stahiki na
kutopata taarifa namna ya kupata rekodi za mashauri.
Lakini
pia hawajui sekta mbalimbali za kisheria zinahusikaje katika uendeshaji
mashauri na utoaji wa haki, kwani andiko lilitarajia kila Mahakama kuwa na
miongozo kwa watumiaji, kuwaongoza wanapotafuta huduma za kimahakama.
Alisema
lugha ya Kiingereza inayotumika mahakamani wakati wananchi wengui wanaotafuta
haki wanatumia Kiswahili, ilitambuliwa katika andiko la WB kuwa moja ya vikwazo
vinavyowazuia wananchi kupata haki.
“Andiko
la WB lilirejea utafiti uliogundua asilimia 60 ya watumiaji wa mahakama
walisema Tovuti za Mahakama hazitoi taarifa za kutosha kuhusu mashauri yao.
“Tovuti
zetu bado hazizungumzi lugha ya Kiswahili, jana nilitembelea Tovuti ya Mahakama
nikakuta nyaraka tano kuhusu suala muhimu la miradhi.
Nayaraka
hizo zimewekwa katika lugha ya Kiingereza lugha ambayo inawatenga watumiaji
wengi wa mahakama., lakini pia imelenga matumizi ya wanasheria zaidi ya
wananchi.Tovuti zetu ziongee lugha ya wananci na ziwe zenye msaada kwa
mwananchi wa kawaida,” alisema Jaji Mkuu Prof. Juma.
Alisema
WB ilionyesha kutambua upungufu wa stadi na utaalamu umepunguza uwezo wa
mahakama kutoka haki kwa weledi na wakati, ambapo andiko lilibaini mfumo wa
upimaji na utendaji unahusu watumishi wasio mahakimu au majaji na hakuna
upimaji kwa Majaji wasajili na mahakimu.
“Kutokuwapo
kwa mfumo wa kupima utendaji wa Majaji, Mahakimu na Wasajili kutaulizwa na WB
katika tathimini yake,” alisema Jaji Mkuu Prof. Juma.
Aliyataja
maeneo mengine yaliyoonyesha wasi wasi wa WB na kuhitajika kufanyiwa kazi ni
pamoja na matumizi madogo ya suluhu nje ya mahakama na upatanishi, gharama za
huduma za mawakili hazidhibitiwi kikamilifu.
Kuwapo
kwa ukubwa wa gharama za madalali kunakofikia hadi asilimia 22 ya thamani ya
mali inayobishaniwa mahakamani.
Awali
Mtendaji Mkuu wa Mahakama Hussein Katanga alisema, zipo changamoto
zinazoikabili mahakama ikiwamo upangaji na uendeshaji wa keshi hususani
mahakama za chini hatua ambayo inahitaji kutiliwa mkazo.
No comments:
Post a Comment