NteghenjwaHosseah,Mbeya
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo amewataka
watumishi wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijiji (Tarura) kuvunja utatu usio
mtakatifu katika kazi za ujenzi na matengenezo ya barabara zinazoendelea kutangazwa
katika maeneo mbalimbali nchini.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo
Ameyasema
hayo wakati wa kufungua mafunzo ya siku Sita ya watalaam wa Tarura kutoka katika
Mikoa saba ya Nyanda za Juu Kusini kuhusiana na masuala ya Ununuzi wa Umma na Usimamizi
wa Mikataba ya Ujenzi na matengenezo ya barabara na Maadili katika kazi za
TARURA yenye takribani miezi Sita tangu kuanzishwa kwake.
Waziri
Jafo amesema "Ninaposema Utatu mtakatifu namaanisha Afisa Manunuzi,
Mhasibu na Mhandisi wa Tarura katika eneo husika hawa ndio huwa wanaamua nani apewe
kandarasi kwa mujibu wa mahusiano na makubaliano wanayoyajua wao."
Huu
Utatu usio mtakatifu katika kazi za Umma ufe kuanzia leo na Mkandarasi apewe kazi
kwa kuzingatia uwezo wake wa kitaalam na kifedha katika kukamilisha kazi hiyo nasio
mahusiano na makubaliano nje ya vigezo vilivyowekwa".
Katika
Utatu huu ninauo uzungumzia kuna mahusiano ya karibu sana na rushwa na ina fahamika
wazi kuwa rushwa hupofusha wataaalam kuona na kutathmini uwezo wa Mzabuni,
huzorotesha kazi iliyopangwa kufanyika na kuwanyima wananchi haki yao ya msingi
ya huduma bora za barabara na tutakaowabaini wakiendeleza kasumba hii tutawachukulia
hatua za kisheria na kinidhamu alisema Jafo.
Akimkaribisha
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala amesema wamejiandaa
kikamilifu kusimamia kazi za Tarura na baada ya uzinduzi wa kitaifa walizindua tena
Kimkoa ili kuwafahamisha wananchi wa mkoa huo umuhimu wa Taasisi hii, ili waweze
kumiliki kazi zinazofanywa na Tarura na kuwaelewesha lengo la kutoka kazi za barabara
kutoka Halmashauri na kusimamiwa na Tarura.
Waziri Jafo (kulia) akiteta jambo
na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala
“Tarura
imekuja kuboresha kazi nzuri iliyokuwa ikifanywa na Baraza la madiwani, Kamati za
kudumu pamoja na Ofisi ya Mkurugenzi sasa TARURA wamekuja kutekeleza kitaalam zaidi,
namna ya usimamizi, manunuzi, mikataba ili tuweze kupata matokea bora na ya haraka.
Naye
Mkurugenzi wa Tarura Eng. Abdul R. Digaga amesema mafunzo
haya ni mpango wa kimkakati wa Tarura katika kupambana na rushwa katika utekelezaji
wa miradi ya ujenzi na matengenezo ya barabara,mgongano wa maslahi, matumizi mabaya
ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi wa barabara na ukosefu wa uadilifu miongoni
mwa watendaji.
Waziri Jafo (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Barabara Vijijini Mhandisi Abdul Digagab
Mafunzo
hayo ambayo yalianza kufanyika katika kanda mbalimbali nchini na kanda hii ya Nyanda
za juu kusini ni ya mwisho kufanyika kwa wataalam wa Tarura wa kada mbalimbali
na imejumuisha Mikoa ya Mbeya, Songwe, Ruvuma, Rukwa, Katavi na Iringa na Njombe.
Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI Selemani
Jafo(aliyekaa katikati) na viongozi wa Mkoapamoja na TARURA na washiriki wa mafunzo
kutoka Mkoa wa Njombe.
No comments:
Post a Comment