ANGELA MSIMBIRA -
LINDI
MGANGA Mkuu wa Mkoa
wa Lindi Ganchwele Makenge ameiagiza timu ya usimamizi wa huduma ya afya wilaya
ya Lindi kuhakikisha wanasimamia na kufuatilia ukarabati wa vituo vya afya ili vijengwe
kwa ubora kulingana na thamani ya fedha zilizo tolewa na Serikali.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Lindi Genchwele Makenge(wa
tano kutoka kulia)
Makenge ameyasema
hayo kwenye kikao cha pamoja kati ya wataalam kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) kwa kushiriana na wataalam kutoka Ofisi ya Mkuu
wa Mkoa na Halmashauri ya Lindi mara baadaya kukagua ujenzi wa kituo cha
afya cha Nyangamara kilichopo kata ya
Nyangamara, wilaya ya Lindi Mkoani Lindi
Makenge amesema Kamati
ya Usimamizi wa Huduma ya Afya inalo jukumu kubwa la kusimamia shughuli zote za
afya katika Mkoa wa Lindi hivyo hawana budi kuhakikisha miradi inayotekelezwa na
Serikali inasimamiwa kikamilifu ikiwepo ya ukarabati wa vituo vya afya nchini.
Amesema kuwa Kamati
hiyo ina hitajika kusimamia wahudumu wa afya katika kuhakikisha wanafanya kazi kwa
kufuata kanuni taratibu na sheria za utumishi wa umma kwa kuwa huduamia wananchi
ipasavyo na kuondoa malalamiko yaliyopo katika sekta ya afya.
Ameiagiza kamati hiyo
kusimamia utendaji ulio bora katika vituo vya afya vya Mkoa wa Lindi kwa kuwahimiza
wafanyakazi kutumia lugha nzuri kwa wagonjwa na kutoa huduma stahiki kwa jamii ili
kuondoa kero mbalimbali ambazo wananchi wamekuwa wakizituhumu katika sekta ya afya
nchini.
Baadhi
ya Wataalam kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(OR-TAMISEMI) pamoja na wataalam kutoka Mkoa wa Lindi wakikagua ujenzi wa jengo
la maabara lililojengwa katika kituo cha afya cha Nyangamara mkoani Lindi.
Kwa upande wake Mganga
Mkuu wa wilaya ya Lindi Bikilo Zuberi amesema kuwa mpaka sasa tayari Serikali imeshatoa
Sh milioni 450 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya mtumishi, Ujenzi wa Maabara,
Chumba cha Upasuaji, wodi ya wazazi na chumba cha kuifadhia maiti jambo ambalo litapunguza
kero kwa wananchi na kuongeza huduma za afya nchini.
Ameishukuru Serikali
kwa kuweza kuboresha huduma za afya katika Mkoa wa Lindi kwa kutoa shilingi milioni
500 kwa ajili ya ukarabati wa kituo cha afya cha Nyangamara kwa kuwa awali kituo
kilikuwa na changamato ya kutokuwa na majengo ya kutosha ya kutolea huduma kwa wananchi
ikiwemo ukosefu wa jengo la maabara, wodi ya wazazi, chumba cha upasuaji,
maabara na chumba cha kuhifadhia maiti.
Baadhi
ya Wataalam kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(OR-TAMISEMI) pamoja na wataalam kutoka Mkoa wa Lindi wakikagua ujenzi wa jengo
la maabara
Wakati huo huo Diwani
wa Kata ya Nyangamara wilaya ya Lindi Mkoani Lindi Ramadhani Malingumu ameipongeza
Serikali ya awamu ya Tano kwa kushirikisha wananchi kwenye ujenzi wa vituo vya afya
nchini jambo ambalo litasaidia katika kutunza na kusimamia vituo vya afya vilivyojengwa.
Aidha amesema wananchi
wa kata hiyo wameshirikishwa katika ujenzi wa kituo hicho kwa asilimia 100 jambo
ambalo linaimarisha ushirikiano kati ya wananchi na serikali katika kuleta maendeleo .
Ujenzi
wa nyumba ya Mtumishi iliyojengwa katika Kituo cha Afya cha Nyangamara kilichopo
Kata ya Nyamara, wilayani Lindi Mkoa wa Lindi.
No comments:
Post a Comment