Na Nteghenjwa Hosseah,
Siha.
WAZIRI
wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo amesema
atafanya kila liwezekanalo kupata fedha zaidi kwa ajili ya ukamilishaji wa
hospital ya wilaya ya Siha.
Waziri
Jafo amesema hayo alipokuwa akifuatilia agizo lake alilolitoa miezi kadhaa iliyopita
ya kuacha kutumia Mkandarasi na kutumia mafundi wa jamii "Force
Account" katika ujenzi wa hospital hiyo ambapo Halmashauri ya Siha ilishatoa
kazi hiyo kwa Mkandarasi na gharama za ujenzi kuwa juu zaidi.
"Katika
ziara yangu iliyopita kazi ilikuwa haijaanza na bado mlikuwa mnajadiliana na Mkandarasi
mlinieleza kuwa zinahitajika fedha zaidi kwa ajili ya kukamilisha kazi hii kwa mujibu
wa Mkandarasi ndipo niliposhauri mtumie mafundi wa kijamii "Force
Account" nasi mkandarasi kama mlivyopanga hapo awali," alisema Waziri
Jafo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo (katikati) akikagua ukamilishaji wa Hospital ya wilaya ya Hai alipofanya ziara yake katika wilaya hiyo.
Aliongeza
"nimefurahi kuwa mlinielewa na mkazingatia ushauri wangu na leo hii ninaona
matunda ya matumizi ya mafundi wa kijamii ambao wamefanya kazi nzuri kwa ubora
wa hali ya juu na gharama nafuu katika hili hongereni sana".
Alisisitiza
kuwa nimeona majengo ambayo yanakaribia kukamilika lakini pia nimeskia taarifa yenu
kuwa bado kuna majengo zaidi ya nahitajika ila kukamilisha hadhi ya hospital ya
wilaya nina ahidi kuwa tafutia fedha kwa ajili ya ukamilishaji wa majengo hayo.
Akisoma
taara ya Afya Mganga Mkuu wa wilaya hiyo Dk. Andrew Method amesema wilaya hiyo
inakabiliwa na changamoto kubwa ya uhaba wa Hospital ya wilaya na vituo vya Afya
vilivyopo ni vitano tu ambavyo kati ya hivyo cha Serikali ni kimoja tu hivyo nguvu
kubwa imewekwa katika kuhakikisha wanapata miundombinu bora ya hospital ya wilaya.
"Fedha
tulizopata ilikuwa ni Sh milioni 200 na kwa kuzingatia maelekezo yako tulitumia
Force Account na kama unavyoona kazi iko katika hatua za mwishoni, ".
Ujenzi
wa Hospital hii utakapo kamilika utawezesha wilaya ya Siha kuwa na hospital moja
ya wilaya pamoja na ile ya Kibong'oto iliyoko chini ya Wizara ya Afya.
Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo akiwa katika picha
ya pamoja na Viongozi wa Mkoa wa Kilimanjaro, pamoja na watumishi wa Halmashauri
hiyo.





No comments:
Post a Comment