Nteghenjwa
Hosseah, TAMISEMI.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi
ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
Selemani Jafo amevitaka Vituo vya Afya nchini sambamba na Hospital za wilaya
kutengeneza bustani za kupumzikia wagonjwa wanaosubiria matibabu katika maeneo
hayo.
Waziri jafo ameyasema
hayo wakati akikagua Ujenzi wa miundombinu ya Afya katika Kituo cha Afya Makole
kilichopo Manispaa ya Dodoma na kuutaka uongozi wa Kituo hicho kutenegenza
bustani ya kisasa pamoja na kupanda miti ya kutosha ili kutunza matunzingira
lakini kupendezesha eneo la hospital.
“Hili Agizo liende kwa
Vituo vyote Nchini pamoja na Hospital za Wilaya zilizoko chini ya TAMISEMI
kuhakikisha wanaekeleza maelekezo haya katika ameneo yote nataka hospital iwe
sehemu ya kupa faraja mgonjwa kwa kupata huduma nzuri lakini pia kusubiria
huduma hiyo katika maeneo yanayovutia wakati wote” Alisema Waziri Jafo.
Akikagua majengo matano
yanayojengwa katika Kituo hicho cha Afya na kusimamiwa na TAMISEMI Waziri Jafo
amesema ameridhishwa na Ujenzi wa miundombinu hiyo ya Afya katika Hospital ya
Makole kwani umefuata ramani
zilizotolewa na Wizara, unajengwa kwa ubora na uko ndani ya muda wa
Utekelezaji.
“Hivi ndio ninavyotaka
wataalamu wangu kujiongeza katika baadhi ya maeneo mfano hapa Mmejenga Mabara
kubwa kulingana na wingi wa wagonjwa mnaowahudumia kwa siku sasa sio kwa sababu
ramani imeonyesha maabara ndogo basi kila mtu anafuata hivyo hivyo ni lazima
tujiongeze kulingana na mahitaji ya ameneo yetu ya huduma” Alisema Waziri Jafo.
Akizungumzia maendeleo
ya mradi Mganga Mfawidhi wa Kituo
cha Afya Makole amesema Ujenzi huu umesema ujenzi wa Maabara,
chumba cha Upasuaji, Wodi ya Kina Mama, Nyumba ya Mganga pamoja na Ukarabati wa
Kichomea Taka utakamilika mapema mwezi February 2017 na Fedha zilizopokelewa
kwa ajili ya ujenzi huo zitatosha na kukamilisha ujenzi wa miundombinu yote.
Kituo cha Afya Makole
ni miongoni mwa vituo 211 Nchini vilivyopokea/vitakavyopokea Fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu
mbalimbali ya Afya lengo ikiwa ni kuboresha Miundombinu ya Afya ili kuweza
kutoa huduma bora kwa watanzania.
TAMISEMI
YA WANANCHI.
No comments:
Post a Comment