Friday, December 29, 2017

SERIKALI imesikia kilio cha wadau wa sekta ya uwindaji wa kitalii nchini na kuamua kuongeza muda wa miaka miwili ya umiliki wa leseni za vitalu 95 vya uwindaji wa kitalii ambazo zilikuwa ziishe muda wake tarehe 31 Desemba mwaka huu (2017).

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wadau wa sekta ya uwindaji wa kitalii katika mkutano uliondaliwa na Wizara yake mjini Dodoma jana kwa ajili ya kujadili mikakati mbalimbali ya kuimarisha sekta hiyo ikiwemo utekelezaji wa azma ya Serikali ya kuanzisha utaratibu mpya wa utoaji wa leseni za vitalu vya uwindaji wa kitalii kwa njia ya mnada. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mej. Jen. Gaudence Milanzi na Naibu Katibu Mkuu, Dk. Aloyce Nzuki (kulia)  

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akisikiliza kwa makini mapendekezo ya wadau wa sekta ya uwindaji wa kitalii katika mkutano uliondaliwa na Wizara yake mjini Dodoma jana. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Gaudence Milanzi.
 KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Mej. Jen. Gaudence Milanzi akizungumza na wadau wa sekta ya uwindaji wa kitalii katika mkutano uliondaliwa na Wizara hiyo mjini Dodoma jana kulia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla
 Baadhi ya wadau wa sekta ya uwindaji wa kitalii wakiwa katika mkutano huo. 
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wadau wa sekta ya uwindaji wa kitalii katika mkutano uliondaliwa na Wizara yake mjini Dodoma jana kwa ajili ya kujadili mikakati mbalimbali ya kuimarisha sekta hiyo ikiwemo utekelezaji wa azma ya Serikali ya kuanzisha utaratibu mpya wa utoaji wa leseni za vitalu vya uwindaji wa kitalii kwa njia ya mnada. Kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mej. Jen. Gaudence Milanzi na Naibu Katibu Mkuu, Dk. Aloyce Nzuki (kushoto kwake). 
 Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Kampuni za Uwindaji wa Kitalii nchini, Michael Mantheakis akizungumza kwenye mkutano huo mjini Dodoma 
  Mdau wa kampuni ya uwindaji wa kitalii nchini, Dk. Ricky Abdallah akichangia kwenye mkutano  
 Baadhi ya wadau wa wakiwa katika mkutano huo.
Baadhi ya watendaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Taasisi zake wakiwa katika mkutano huo.

No comments:

Post a Comment