Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Seleman Jafo amesema hatavumulia kuwa na watumishi mizigo ambao hawatimizi majukumu yao kikamilifu na kuleta mabadiliko katika sekta ya barabara ambayo ni nguzo ya uchumi nchini.
Waziri Jaffo aliyasema hayo wakati wa ufunguzi wa semina ya siku moja kwa wabunge wa Kamati ya kudumu Serikali za Mitaa (TAMISEMI) sambamba na Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa(LAAC) kuhusu majukumu ya Wakala wa barabara za vijijini na mijini (TARURA) iliyofanyika katika ukumbi wa Hazina Mjini Dodoma.
Mkurugenzi
Mtendajiwa Wakalawa Barabara Vijijini na Mjini Mhandisi Victor Seif akieleza majukumu
ya TARURA kwenye kikao cha Kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za
Mitaa na Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa mjini Dodoma.
Waziri Jaffo amesema Serikali ilishatoa muongozo wa malengo
ya utendaji kazi katika utumishi wa umma na kuwapima kulingana na malengo yao hivyo
watumishi ambao watashindwa kutekeleza na kufikia malengo waliyopangiwa Serikali
haitasita kuwachukulia hatua za kiutumishi.
Amesema kuwa Serikali haitavumilia suala zima la ubadhilifu
kwa watumishi wa umma, kwa kuwa Serikali haiwezi kumbeba mtu ambaye ni mbadhilifu
kwa kuwa Serikali ina hitaji kuleta mabadiliko katika utendaji kazi na kuleta maendeleo
kwa jamii.
AmesemakuwaTaruaranichombokipyahivyohaitajikuajiriwatumishiambaonimzigoambaowaletasurambayakwajamiikablachombohikihakijafanyakaziyakuwahudumiawananchikatikakutatuakeroyamiundombinuyabarabaravijijininamijini.
Amewataka Wabunge wa kamati zote mbili (LAAC & TAMISEMI)
kusimamia utekelezaji wa miradi iliyoko chini ya TARURA na kuhakiki ubora wa miradi
hiyo na kukosoa pale wanapoona miradi haitekelezwi
kwa viwango vinavyotakiwa ili wahusika waweze kurekebisha makosa kabla ya kukabidhi
miradi hiyo kwa wa husika.
Aidha aliwahisi Wabunge kuendelea kuishauri TARURA kwa kuwa
chombo hicho kimeundwa kwa ajili ya kutoa majibu ya changamoto za Wananchi hivyo
ni wajibu wetu kuwasilisha yale yote ambayo tunaona yanawakwaza wananchi katika
majimbo yetu.
Jaffo amemuagiza Mkurugenzi wa TARURA Mhandishi Victor Seif kuhakikisha Mameneja katika ngazi ya Wilaya wanasaini
Mkataba wa Makubaliano ya kazi “Performance contract” na kuwafuatilia
utendaji wao kwa mujibu wa Mkataba na atakeyeshindwa kufikia malengo yaliyowekwa
atolewe bila kigugumizi ili kupisha watendaji wengine watakaofanya kazi kulingana
na matakwa ya Serikali.
Wakati huo huo Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa barabara vijijini
na mijini (TARURA) Mhandisi Victor Seif amesema kulingana na muundo na majukumu
ya Wakala wa Barabara mahitaji halisi ya watumishi ni 3,222 lakani mpaka sasa ni
watumishi 1,147 wameshapatika na ambapo 47 wako Makao Makuu, 103 mikoani 997
katika halmashauri, na pia kuna upungufu wa watumishi 2,075 katika kada mbalimbali.
TARURA ina majukumu ya
msingi ya ujenzi, ukarabati na matengenezo ya mtandao
wa barabara zenye urefu wa Km 108,946.2 za vijini, mijini pamoja na madaraja,
na kati ya hizo barabara 56,000 zinafanyiwa uhakiki ili ziweze kutangazwa kwenye
Gazeti la Serikali ili zitambulike kisheria na Km 52,946.2 tayari zimeshatambulika
na kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali.
No comments:
Post a Comment