baadhi ya maboksi yakiwa na vifaranga vilivyoteketezwa
kwa moto
WATETEZI wa haki za wanyama na ndege wamelaani uamuzi wa kuchomwa moto kwa vifaranga zaidi ya 6,000 wakisema ulikuwa wa kikatili zaidi usio na utu wala ubinadamu.
Wizara ya mifugo kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Arusha juzi viliteketeza vifaranga wenye thamani ya Sh milioni 12 waliodaiwa kuingizwa kinyume cha sharia, kupitia njia za panya mpaka wa Namanga, wilayani Longido.
Akizungumza ofisini kwake Mkurugenzi Mtendani ya Shirika lisilo la kiseriali la ‘The Arusha Society Protection of Animals’ (ASPA), Livingstone Masija alisema, zoezi hilo lilikuwa la kikatili.
Gari linalodaiwa kubeba vifaranga waliokamatwa katika Mpaka wa Namanga wilayani Longido mkoani Arusha
Maboksi ya vifaranga hai yakishushwa tayari kwa kuteketezwa
Masija akielezea kuhusu zoezi la
kuwaangamiza vifaranga hao alisema, licha ya kuwapo kwa sheria zinazosimamia
katika mazingira ya viumbe kama wale bado ubinadamu ulihitajika zaidi katika
kutekeleza sheria husika.
“Maamuzi yaliyochukuliwa ni ya
kikatili zaidi tunajua sheria zipo, na lazima zizingatiwe lakini pia kuwe na
ubinadamu katika kutekeleza majukumu ya kisheria,” alisema Masija na kuongeza:
“Kuna utaratibu wa kutekeleza jambo
kama hili kwetu sisi watetezi wa haki za wanyama huwa tunazingatia haki au
misingi ya wanyama,” alisema.
Alisema, kila mnyama au ndege wa
kufugwa anayo haki ya kuishi na panapohitajika kumuua ipo njia bora ya
kumteketeza badala ya kutumia njia za kikatili kama ilivyofanywa kwa vifaranga
vya kuku.
“Yale ni mauaji ambayo kwa ujumla
hayastahili wala hayawezi kuvumilika kitaifa wala kimataifa. Ustaarabu wa taifa
lolote pia huonekana kwa namna ya watu wanavyoishi na wanyama na ndege
wanavyofugwa.”
Alisema japokuwa bado hakujawa na
taarifa sahihi zilizolipotiwa kuwa vifaraga hao walikuwa na magonjwa kama mafua
ya ndege lakini hata kama wangekutwa na maambukizi hayo bado njia ya
kuwaangamiza haikuwa sahihi.
“Pamoja na changamoto za magonjwa
bado walitakiwa kutafuta njia sahihi za kujiridhisha kama vifaranga walikuwa na
matatizo ya kiafya.
“Na hata kama wagegundulika kuwa na
mafua ta ndege bado huwezi kuchukua hatua ya kuwateketeza kwa moto zipo njia
sahihi za kistaarabu na si ukatili,” alisema Masija.
Aliitaja njia ya kwanza inayoweza
kutumika kutetekeza vifaranga hao kwamba ilipaswa kuwapunguzia maumivu kabla ya
kuwateketekeza kwa kuwapulizia dawa yenye usingizi kisha wakalewa.
“Ndege kama vifaranga wale walipaswa
kupuliziwa dawa itakayowalewesha kisha wakafa wenyewe usingizini, baada ya hapo
ndipo zingefuata hatua za kuwafukia au kuteketeza kama miziga badala ya
kuwachoma wakiwa hai,” alisema Masija.
Akifafanua kuhusu sheria na taratibu
nyingine Masija alisema, hata kama vifaranga hao waliingizwa kinyume cha sheria
bado namna bora iliyopaswa kufanywa ilikuwa ni kuvirudisha vilikotoka.
“Vile vifaranga si vipodozi au
maboksi ya dawa wale ni viumbe hai walipaswa kwenda mbele zaidi ya uamuzi
walioufanya,” alisema Masija.
Akizungumza juzi baada ya kukamatwa
kwa vifaranga hao Afisa Mfawidhi Mkaguzi wa mifugo kutoka Kituo cha Forodha
kilichopo Namanga Medadi Tarimo alisema, vifaranga hivyo walikamatwa usiku Saa
3 na vyombo vya ulinzi na usalama.
Alisema mara baada ya kukamatw akwa
vifaranga hivyo iliwalazimu kuviteketeza ili kulinda afya za binadamu kwa
mujibu wa sheria ya wanyama ya mwaka 2003 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2007
ikiwa ni sehemuya mkakati wa kukabiliana na mlipuko wa mafua ya ndege katika
nchi mbalimbali.
No comments:
Post a Comment