Saturday, September 16, 2017

UZINDUZI WA MRADI WA KUJENGA UWEZO WA JAMII YA VIZIWI NA UWAJIBIKAJI KWA UMMA KATIKA JIJI LA ARUSHA SEPTEMBA 16, MWAKA 2017 CHINI YA UFADHILI WA THE FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY KUPITIA CHAMA CHA VIZIWI TANZANIA (CHAVITA).


Watatu kutoka kulia ni Katibu Tarafa ya Themi Halmashauri ya Jijini la Arusha akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi Viziwi kutoka Shule ya Msingi Meru, Maofisa wa CHAVITA mkoa na Taifa na baadhi ya watumishi wa Jiji baada ya ufunguzi wa mradi wa kujenga uwezo wa jamii ya Viziwi na uwajibikaji kwa umma katika Jiji la Arusha hafla iliyofanyika kwenye Viwanja vya Makumbusho Arusha  
Baadhi ya wanafunzi viziwi kutoka Shule ya Msingi Meru jijini Arusha wakiwa wameshika mabango yenye jumbe mbalimbali wakati wa uzinduzi rasmi wa mradi wa kuwajenga uwezo wa jamii ya Viziwi na uwajibikaji kwa umma jijini Arusha  

Wadau wenye tatizo la kuskia (viziwi), wakiwa wameshika mabango yenye ujumbe muhimu wakati wa uzinduzi wa mradi wa kujenga uwezo katika jamii ya viziwi na uwajibikaji kwa umma 

 Afisa Jinsia wa Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA), Lupi Maswanya akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa kujenga uwezo wa jamii ya Viziwi na Uwajibikaji kwa umma katika Jiji la Arusha, katika uzinduzi huo alimuwakilisha Mkurugenzi wa CHAVITA Tanzania.

Maofisa Ustawi wa Jamii kutoka Halmashauri ya Jiji la Arusha kutoka kulia ni Novo Kikaho, Nancy Matee na Irene Kombe wakifuatilia hotuba wakati wa uzinduzi wa mradi wa kujenga uwezo wa jamii ya Viziwi na uwajibikaji kwa umma katika Jiji la Arusha 


Baadhi ya wadau waliohudhuria uzinduzi wa mradi huo katika Viwanja vya Makumbusho ya Azimio la Arusha mjini hapa



Maofisa wa Chama cha Viziwi Tanzania CHAVIWATA wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi wakati wa uzinduzi wa Mradi wa kujenga uwezo kwa jamii ya Viziwi na uwajibikaji kwa umma katika Jiji la Arusha 

No comments:

Post a Comment