Monday, August 21, 2017

UZINDUZI WA MRADI WA UMEME VIJIJINI (REA) AWAMU YA TATU

UZINDUZI WA MRADI WA UMEME VIJIJINI AWAMU YA TATU KATIKA KIJIJI CHA DIGODIGO WILAYANI NGORONGORO MKOANI ARUSHA UMEZINDULIWA NA NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI DK. MEDARD K. KALEMANI (MB), AGOSTI 19, 2017


Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dk. Medard Kalemani akikata utepe wa kuzindua rasmi kwa mradi wa awamu ya tatu ya umeme vijijini katika Kijiji cha Digodigo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha, kushoto ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa Jimbo hilo William Ole Nasha akifuatiwa na Mkuu wa wilaya hiyo Rashid Taka  
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dk. Medard Kalemani akifungua kitambaa kwa ajili ya kuzindua rasmi mradi huo katika Kijiji cha Digodigo, Kata ya Digodigo Tarafa ya Sale wilayani Ngorongoro mkoani Arusha

Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dk. Medard Kalemani akibonyeza kitufe chenye King'ola kuzindua rasmi mradi wa umeme vijijini katika Kijiji cha Digodigo, Kata ya Digodigo Tarafa ya Sale wilayani Ngorongoro mkoani Arusha
Viongozi waliohudhuria uzinduzi huo wakipiga makofi kuashirikia kukamilika kwa shughuli hiyo iliyofanyika Kijiji cha Digodigo Kata ya Digodigo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha
 Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha Rashid Taka akibonyeza King'ola kuashiria uzinduzi wa mradi wa umeme vijijini katika Kijiji cha Digodigo wilayani humo.

No comments:

Post a Comment