IMEELEZWA kuwa utoroshwaji wa madini ya
Tanzanite katika mgodi wa Tanzanite One wilayani
Simaniro mkoani Manyara umesababishwa na kutokuwepo kwa
kituo cha cha kuuzia madini ( EPZ) jambo ambalo limeisababishia
Halmashauri ya Wilaya hiyo kukosa mapato yanayotokana na madini.
Akizungumza na wadau wa madini Mkoa wa Manyara Naibu
Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani alisema kuwa ili
kuthibiti utoroshwaji huo wa madini ya Tanzanite One Serikali
imeamua kujenga Kituo hicho cha Kuuzia madini EPZ Wilayani simanjiro
Mkoani Manyara.
“Serikali imedhamiria kujenga kituo kikubwa cha
kuuzia Madini yetu ya Tanzanite One ili
kudhibiti utoroshwaji wa madini hayo hivyo
sasa madini yote yatasanifiwa hapa nchini, Haitaruhusiwa
kusafirisha vito ghafi nje ya nchi” Alisema
Dkt Kalemani.
Alisema kuwa Wameamua kudhibiti Tanzanite One ili
iwanufaishe wananchi wa eneo husika na watanzania
wote hivyo kila mtu ana wajibu na jukumu la
kuyalinda madini hayo ili yasitoroshwe.
Aidha aliwataka wachimbaji wote pamoja na makampuni
yaliopo katika Mgodi huo wa Mirerani kulipa kodi ndani ya siku
saba kuanzia taerehe 24 juni ya services
lavey ambayo ni asilimia 0.3 ya halmashauri
husika ikiwa ni pamoja na malimbikizo ya nyuma.
Dkt Kalemani alisema kuwa biashara ya wachimbaji
wakati na wachini inapaswa kutolewa kwa watanzania pekee ambao ni
wazawa na si wageni kutoka nje ya nchi na kueleza kuwa biashara hiyo
kwa sasa imetawaliwa na raia wanchi jirani ya Kenya ambapo ni
kinyume na sheria ya nchi.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Zephania Chaula
alisema kuwa wachimbaji wa madini pamoja na wafanyabiasha wamekuwa
wakikwepa kulipa kodi kitendo ambacho kinaisababishia Halmashauri
upotevu wa mapato yake ya ndani .
“Wachimbaji wapo Zaidi ya 2000 lakini hawalipi
kodi mpaka tuanze kukimbizana , naombeni jamani wale
wenye makampuni lipeni kodi, na kama kuna uwezekano wa
kuyafungia makampuni ambayo hayalipi kodi
tuyafungie” Alisema DC Simanjiro.
Naye Mkurugenziwa Halmashauri ya Wilaya hiyo ya SimanjiroYefred
Myenzi alieleza kuwa biashara ya madini katika mgodi huo imegubikwa
na usiri mkubwa na utoroshwaji matokeo yake halmashauri
inanpoteza mapato ya services lavey hivyo aliomba
biashara hiyo ifanyike mererani ili kuondoa utoroshwaji
na usiri uliopo sasa.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha
wachimbaji madini Mkoa wa Manyara( MAREMA) Bw, Sadick Mnene alisema
kuwa uzalishaji wa madini kwa sasa umepungua kutokana na ukosefu wa
baruti hivyo wanaiomba STAMICO kuwasaidia upatikanaji wa baruti
na pia kitalu block B na D madini
yamepotea hivyo serikali ifanye uchunguzi na kujua umbali wa madini
.
No comments:
Post a Comment