KAMPUNI
ya usafiri wa ndege ya flydubai (www.flydubai.com) yenye
afisi zake Dubai imetangaza mwanzo wa safari za ndege zake kutoka Dubai hadi Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro, Tanzania.
Safari
hizo zinatarajiwa kuanza Oktoba 29, Mwaka huu. Huku huduma hiyo ikimaanisha
kuwa kampuni hiyo, licha ya kuwasafirisha wateja hadi Jijini Dar es Salaam
na Zanzibar, sasa itakuwa na vituo 12 barani Afrika.
Taarifa
ya Kampuni hiyo kwa vyombo vya habari Juni 15, Mwaka huu imesema, Uwanja wa
ndege wa Kilimanjaro utakuwa kituo cha tatu nchini Tanzania na cha 12 miongoni
mwa vituo vyote vya flydubai Afrika.
“Huduma hii mpya imeongeza safari za ndege kutoka Dubai kwenda
Tanzania kufikia 14 kwa wiki. Safari za moja kwa moja kutoka Dubai kwenda
Zanzibar zitaongezeka zaidi ya mara dufu kuanzia Oktoba 29, Mwaka 2017,”
ilisema taarifa hiyo.
flydubai ilianzisha operesheni zake Tanzania Mwaka 2014 na
imepata ongezeko kuu la wasafiri kwa miaka michache iliyopita. Uwanja wa ndege
wa Kilimanjaro utapata safari Sita kwa wiki na tatu miongoni mwake zitakuwa
kupitia kwa Jiji Kuu la Dar es Salaam.
Zaidi ya hayo, kampuni hii itaongeza safari za moja kwa moja
toka Dubai hadi Zanzibar kutoka tatu had inane kwa wiki.
Akiongea kuhusu safari hizi, Afisa Mkuu Mtendaji wa Kampuni ya
flydubai, Ghaith Al Ghaith, amesema: “Kutokana na kuongezwa kwa huduma za
usafiri hadi uwanja wa Kilimanjaro pamoja na safari zaidi za moja kwa moja hadi
Zanzibar, kampuni yetu itatekeleza safari 14 kila wiki, ambalo ni ongezeko
la asilimia 133% kwenye huduma hizo ikilinganishwa na mwaka uliopita.Hili ni
dhihirisho bora kwamba umaarufu wa Tanzania kama kituo cha watalii umeongezeka
na tuna furaha kuwasafirisha wateja wetu kwenda na kutoka Dubai.”
Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro upo kati ya maeneo ya Kilimanjaro na
Arusha Kaskazini mwa Tanzania. Uwanja huo ndio kiingilio cha eneo la
Kilimanjaro ambalo linajumlisha maeneo ya Mlima Kilimanjaro, Hifadhi ya
Wanyama-Pori ya Arusha, Ngorongoro Crater na Hifadhi ya wanyama-Pori ya
Serengeti. Ni kampuni chache tu za usafiri wa ndege za kimataifa ambazo hutoa
huduma kwa eneo la Kilimanjaro – na kampuni ya flydubai ndiyo ya kwanza kutoa
huduma hii moja kwa moja kutoka eneo la Milki ya Kiarabu ya UAE.
“Tumejitolea
kutoa huduma za usafiri kwa sehemu ambazo zina uhaba wa huduma hizo. Na huduma
za kampuni ya flydubai kwenye uwanja wa Kilimanjaro itawapa wasafiri nafasi za
kusafiri baina ya kitengo vya Biashara (Business Class) na kitengo cha Uchumi
(Economy Class).
“Kadhalika,
tumewapa wasafirishaji nafasi zaidi za kusafirisha mizigo kupitia kwa idara
yetu ya usafirishaji wa mizigo. Tunatarajia kuona usafirishaji bora wa
kibiashara na wa watalii katika safari hizi kutoka eneo la GCC na eneo la Uropa
Mashariki kupitia kituo cha Dubai,” akasema Sudhir Sreedharan, ambaye ni Kaimu
Mkuu Makamu wa Rais wa kampuni anayesimamia kitengo cha Biashara (eneo la GCC
na Bara la Afrika).
Kampuni
ya flydubai ilipata ongezeko la aslimia 3.5% ya wasafiri kutoka UAE na Afrika
katika mwaka wa 2016 ikilinganishwa na mwaka wa 2015 – ambalo ni dhihirisha
kuwa usafiri kuelekea eneo la Afrika unazidi kunawiri.
flydubai
imetekeleza usafiri murua Barani Afrika kwa kuhudumia maeneo ya Addis Ababa,
Alexandria, Asmara, Djibouti, Entebbe, Hargeisa, Juba, Khartoum, Port Sudan na
hata maeneo ya Dar es Salaam, Kilimanjaro na Zanzibar. Vituo hivi vyote 12
vitahudumiwa kwa jumla ya safari 80 kila wiki wakati wa msimu huu wa kiangazi.
Kwa
habari kamili kuhusu huduma na nauli za usafiri, tembelea: www.flydubai.com/en/plan/timetable.
APO kwa niaba ya flydubai.
No comments:
Post a Comment