WAKULIMA
wa
zao la Shayiri nchini wametakiwa kuendelea kufuata kanuni na maelekezo kutoka
kwa wataalamu ili wavune shayiri nyingi kwa ekari moja na yenye ubora
unaotakiwa.
Ushauri huo ulitolewa wilayani Karatu mkoani hapa hivi
karibuni na Mkuu wa kitengo cha kimea cha SBMiller, Thinus Van Schoor kwa
wakulima wa Shayiri wanaoendesha kilimo cha zao hilo katika wilaya zilizopo
Mkoa wa Arusha na Manyara.
Akizungumza na wakulima hao Van Schoor alisema, ili
wakulima hao waweze kufikia viwango vya uzalishaji wa shayiri bora kutoka
shambani wanawajibu wa kufuata maelekezo na ushauri wa watalaamu.
Alisema wakiwa wanaadhimisha Siku ya Mkulima wa Shayiri,
wanaowajibu wa kuendelea kutumia mbegu bora, mbolea, kupulizia dawa na kupanda
kwa wakati hatua itakayowawezesha kuvuna mavuno mengi kwa ekari kama
walivyofanya mwaka 2015.
“Mwaka 2015 mmefanikiwa kuzalisha Shayiri ya kutoka hii ni
tofauti kabisa na miaka mingine TBL inachukua fursa hii kuwapongeza. Tunasisitiza
muendelee kusikiliza wataalamu ili mzidi kufikia mafanikio zaidi ya haya,”
alisema Van Shoor na kuongeza:
“Mafanikio haya yanayonesha kila mtu anaweza kufanya vizuri
akifuata maelekezo, mmefanikiwa kuwa na Kilogram 686 kwa Ekari katika kwa mwaka
jana haya ni mafanikio kwetu pia,” alisema.
Kwa upande wake Mshauri Mwelekezi wa kilimo cha Shayiri
kutoka TBL Dk. Bennie Basson alisema kwa Mwaka 2013 wakulima wa Shayiri
walilipwa kiasi cha Sh. Bilioni 7.5, Mwaka 2014 Sh. Bilioni 12 na Mwaka 2015 walilipwa
Sh. Bilioni 15.3.
Alisema katika uwiano wa malipo hayo ni wazi kwamba kila
mkulima moja kwa mwaka 2013 alilipwa Sh. 261,000 kwa ekari moja, Mwaka 2014 alilipwa
Sh. 300,000 kwa ekari na Mwaka 2015 mkulima huyo alilipwa Sh. 680,000 kwa ekari.
Naye Mkulima wa Shayiri kutoka Monduli Juu Meporoo Leluse
alisema katika msimu wa kilimo wa mwaka huu ameweza kulima Ekari 235 hata hivyo
hana matumaini ya kuvuna kama alivyofanikiwa mwaka jana kutokana madai kwmba mvua
ilikuwa kubwa.
“Mwaka jana nililima ekari 235 za Shayiri nikavuna gunia 11
kwa kila ekari moja. Mwaka huu sina matumaini sana kwasababu baada ya mvua
kukatika jua liliwaka na wadudu wakavamia kwa wingi, hata ukipuliza dawa bado
hawafi,” alisema Meporoo.
No comments:
Post a Comment