NA ELIYA MBONEA, ARUSHA.
JINA la Mchungaji Emmanuel Alifora Munisi limetajwa katika
orodha ya mashahidi 41 wa upande wa Mashitaka katika kesi ya utakatishaji
fedha, inayomkabili Wakili Medium Mwalle na wenzake watatu.
Watuhumiwa katika kesi hiyo iliyofunguliwa Mwaka 2011 ni Wakili
Mwale, aliyekuwa Meneja wa CRDB Tawi la Mapato jijini Arusha, Boniphace Thomas,
Elias Ndejembi na Don Bosco Gichana mfanyabiashara wa jijini Nairobi nchini
Kenya.
Januari 21, Mwaka huu, Wakili wa Serikali Mkuu Oswald
Tibabyakomya akisaidiana na Felix Kwetukia aliwasomea watuhumiwa mashitaka 42,
mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mustapha Siyani wa Mahakama ya Hakimu Mkazi
Arusha.
Wakili wa Serikali alidai kwamba, mashitaka yanayowakabili
watuhumiwa hao ni utakatishaji wa fedha. Kugushi nyaraka na kukutwa na mali
zilizopatikana kwa njia ya uhalifu.
Mbali na mashitaka hayo, Wakili wa Serikali alitaja majina
ya mashahidi 41 wa upande wa mashitaka watakaotoa ushahidi pindi kesi hiyo itakapoanza
kusikilizwa Mahakama Kuu, kutokana na Mahakama ya Hakimu Mkazi kutokuwa na mamlaka
ya kisheria ya kusikiliza kesi hiyo.
Mashahidi waliotajwa katika kesi hiyo ni Mch. Munisi,
watoto wawili wa Wakili mwandamizi jijini Arusha Loomu Ojare ambao ni Arold
Loomu Ojare na Eliufoo Loomu Ojare.
Wengine waliotajwa kutoa ushahidi wao ni Charles Edward
Obaa, Fatuma Abdul, Shukran Basaemela,Winston Makuri, Janeth Kileo, Agnes
Ngalo, Stella Byabato, Judith Lubuva, ASP Fadhil Mndemu, Seleman
Nakulinga,Balainesh Issa na Doroth Muro
Wakili huyo aliendelea kuwataja mashahidi wengine kuwa ni
Andrew Maganga,Abdallah Muksin,Said Nassoro, Mejooli Mollel,Joseph
Kivuyo,Emanuel Mathayo,Migangala Mirenge, Seif Marwa, Julius Ole Sekeyan,
Charles Chilala, Bakari Musa na Abubakar Haji, Abdallah Khalid.
Wengine waliotajwa ni Mariko Mwairwa, Rashid Kapwani, Steven
Paul, Dk.Najib Msenga, Benjamin Komba, Godfrey Elias, Julius Marwa, John
Mdachi, ,Ibrahim Saidi,Valentine Masawe na Allan Pekins.
Katika kesi hiyo Wakili Omar Juma anamtetea mtuhumiwa wa kwanza
na wa pili ambao ni Wakili Mwale na Gichana, mtuhumiwa wa tatu Thomas anatetewa
na Wakili Albert Msando na mtuhumiwa wa nne Ndejembi anatetewa na Wakili Moses
Mahuna.
Kesi hiyo imepangwa kuendelea Februari 2, Mwaka huu ambapo
upande wa Jamhuri utaendelea kuwasilisha vielelezo ambavyo vitawasilishwa
Mahakama Kuu wakati kesi hiyo itakasikilizwa.
Mwisho
No comments:
Post a Comment