BODI ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) ikiongozwa na Mwenyekiti wa bodi Jenerali Mstaafu George Waitara imetembelea Hifadhi ya Taifa ya Katavi kwa ajili ya kukagua utendaji kazi.
Mbali ya ukaguzi huo Bodi hiyo pia ilipata fursa ya kupokea
taarifa kutoka kwa Mkuu wa Hifadhi Izumbe Msindai.Ambapo Bodi hiyo ilipongeza
utendaji kazi katika Hifadhi ya Katavi hususani kupambana na ujangili na juhudi
zinazofanywa katika kuongeza idadi ya watalii hifadhini.
Aidha, Jenerali Waitara aliutaka uongozi wa hifadhi kuongeza
jitihada katika kukabiliana na changamoto za mifugo ambayo ni kubwa kwa Katavi
na pia alipongeza uongozi wa mkoa chini ya Mkuu wa Mkoa Meja Jenerali mstaafu
Raphael Muhuga kwa ushirikiano mkubwa anaotoa kwa hifadhi katika kupambana na
mifugo hifadhini.
Mapema kabla, bodi iliweza kutembelea kituo cha mafunzo cha
Mlele na kupokea taarifa kutoka kwa Mkuu wa Kituo Mhifadhi Genes Shayo na
kupata nafasi ya kuongea na askari wapya wanaoendelea na mafunzo katika kituo
hicho.
Jenerali Waitara aliwataka askari hao kuwa na nidhamu,
uwajibikaji, bidii na uzalendo katika mafunzo yao na kuwa ni lazima waonyeshe
kuiva ili waweze kupambana vilivyo na changamoto ya ujangili katika Hifadhi za
Taifa nchini.
No comments:
Post a Comment