UFUNGUZI WA NYUMBA ZA KUISHI ASKARI MAGEREZA, GEREZA KUU LA ARUSHA LILIPO ENEO LA KISONGO UMEFANYWA NA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI MWIGULU LAMECK NCHEMBA.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba akisalimiana na Maafisa wa Jeshi la Magereza wakati wa uzinduzi wa nyumba Tano za kisasa za askari wa Gereza Kuu la Arusha lililopo Kisongo mjini hapa, ambapo nyumba hizo zimejengwa na Shirika la Magereza kwa gharama ya Sh. Milioni 50 kila nyuma na hivyo kugharimu Sh. Milioni 253.9.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba akisalimiana na Kamanda wa Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) anayeshughulia wafungwa wa iliyokuwa Mahakama ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda Saidou Guindo
Kamishna Jenenrali wa Magereza nchini Dk. Juma Malewa akizungumza wakati wa uzinduzi wa nyumba za askari katika Gereza Kuu la Arusha lililopo eneo la Kisongo
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba akikagua nyumba za askari magereza zilizojengwa Gereza Kuu la Arusha eneo la Kisongo, kushoto ni Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dk. Juma Malewa, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Arusha Hamis Nkubas na Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema (Chadema).
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba akikata utepe kuzindua rasmi nyumba tano za askari magereza zilizojengwa Gereza Kuu la Arusha eneo la Kisongo, pembeni yake ni Mbunge wa Jimbo la Arusha (CHADEMA), Godbless Lema na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dk. Juma Malewa.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa wa Magereza wakiwamo pia mafundi waliojenga nyumba hizo wakati wa uzinduzi rasmi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Lameck Nchemba akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Arusha pamoja na maofisa wa Magereza nchini na Mbunge wa Jimbo la Arusha (CHADEMA), Godbless Lema.
No comments:
Post a Comment