Na JANETH MUSHI ,
-ARUSHA
SAKATA la dhamana ya Mbunge wa Arusha Mjini(Chadema),Godbless Lema limeendelea kuchemsha “bongo” za Mawakili wa pande zote mbili baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kutoa uamuzi kuwa Mbunge huyo ana haki ya kukata Rufaa.

Uamuzi huo ulitolewa
baada ya Mawakili wa Serikali kuwasilisha hoja za kisheria za pingamizi Novemba
17, Mwaka huu, wakipinga Mahakama Kuu kusikiliza maombi ya dhamana
yaliyowasilishwa na Mawakili wa Lema.
Awali kabla ya kutoa
uamuzi huo jana mjini hapa Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Jaji Sekela
Moshi aliazilimika kuwaita Mawakili ndani “Chamber Court’, hata hivyo kutokana
na wingi wa watu alilazimika
kulipeleka shauri hilo Mahakama ya wazi (Open Court).
Akitoa uamuzi huo
Jaji Moshi alikubaliana na hoja ya Wakili
wa Serikali Paul Kadushi, kuwa mshitakiwa alitakiwa atumie haki yake
kukata rufaa kupinga uamuzi wa Mahakama ya chini badala ya kuiomba
Mahakama Kuu ifanye mapitio ya majalada ya kesi hizo.
Jaji Moshi alikubaliana na hoja ya pili ya Wakili Kadushi aliyedai maombi ya Lema hayakuwa yamekidhi matakwa ya kisheria chini ya kifungu cha 359(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai sura ya 20 kama ilivyofanyiwa marejeo Mwaka 2002.

Kifungu hicho kinachoelekeza
mtu asiporidhika na uamuzi wa Mahakama
ya chini, anatakiwa kukata rufaa Mahakama Kuu.

“Wakili Kadushi
alidai mshitakiwa hajaonyesha chochote
kitakacho halalisha Mahakama ifanye marejeo. Huku Wakili Peter Kibatala wa Utetezi, akisema mshitakiwa asingeweza kukata
rufaa kwa sababu amri iliyotolewa
mahakama ya chini haiwezi kukatiwa rufaa,” alisema Jaji Moshi akinukuu hoja
zilizotolewa na Mawakili hao.
Jaji Moshi aliendelea kueleza kwamba uamuzi wa mahakama ya chini unaolalamikiwa unaangukia
kuanzia kifungu cha 148 hadi 160 vya Sheria ya
Mwenendo wa Makosa ya Jinai.
Ambapo kifungu cha
161 cha sheria hiyo hapo juu, kinaelezea maamuzi
yanayotolewa chini ya vifungu hivyo ambavyo vinashughulikia dhamana kuwa vinaweza kukatiwa rufaa.
“Nimetilia maanani hoja hizi, naona ni wazi kwamba maombi haya yanaweza kukatiwa rufaa na haki ya kukata rufaa haiondoi haki ya
marejeo.Pande zote mbili sheria inataka mtu ambaye hajaridhika na
uamuzi akate rufaa au atoe sababu ya kuifanya Mahakama ifanye
marejeo,”alisema Jaji Moshi na kuongeza:
“Nilivyoangalia kwa kuwa vifungu hivyo vinaweza kukatiwa rufaa, mshitakiwa alitakiwa atumie haki yake kukata rufaa.Nakataa ombi
la kufanya marejeo ambayo Mahakama iliyafungua baada ya kupitia
malalamiko ya Lema, nayafuta na nina amuru hivyo,” alisema.
Jaji aliendelea kusema kuwa Mahakama hiyo iliwaita wadaawa wa
pande zote mbili Novemba 17, Mwaka huu, ambapo hoja ya kwanza ya
mawakili wa serikali ilikuwa ni Mahakama hiyo haiwezi kufanya marejeo
au masahihisho ya mwenendo wa kesi ya mahakama ya chini.
Jaji Moshi alikataa hoja hiyo ambapo mawakili wa serikali walidai
kifungu cha 372 (1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ambacho
kinaipa Mahakama Kuu kufanya mapitio ya mashauri ya kesi za mahakama
za chini,ila baada ya mabadiliko ya kisheria yaliyofanyika Mwaka 2002
yaliondosha haki za pande zozote katika kesi za jinai kuomba rufaa au
mapitio ya maamuzi madogo yaliyofanywa katika mahakama za mahakimu
nchini.
Mawakili hao walidai kwa mujibu wa kifungu cha 43(2) cha
Sheria ya Mahakama za Mahakimu,maombi hayo yanakinzana na kifungu
hicho kwani uamuzi huo mdogo unaopingwa na Mawakili wa Lema
haujamaliza shauri la Jinai katika Mahakama ya chini.
“Naona hoja ya kuwa mshitakiwa angezingatia kifungu cha 43(2) ni hoja
ambayo si sahihi, sitaenda kuzungumzia kifungu hicho. Hivyo hoja hiyo
siikubali na naitupilia mbali na nimetilia maanani hoja za pande zote
kwani mahakama ndiyo iliwaita ili waje wafafanue malalamiko na ijiridhishe iwapo itafanya marejeo au la,” alifafanua Jaji Moshi
Jana Serikali iliwakilishwa na Wakili Mwandamizi Matenus Marandu
akisaidiana na Elizabeth Swai huku Lema akitetewa na Wakili Peter
Kibatala, akishirikiana na Adam Jabir, Sheck Mfinanga na Faraji
Mangula.
Akizungumzia uamuzi huo Wakili kibatala alidai kuwa wanataka rufaa
kama walivyoelekezwa na mahakama ambapo wataikata chini ya hati ya
kiapo.

Jalada la maombi
hayo lilifunguliwa na Mahakama Kuu chini ya kifungu cha 372 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, baada kupokea
malalamiko kutoka kwa mshitakiwa kupitia
mawakili wake, ili iweze kujiridhisha na uamuzi uliolalamikiwa.
Kutokana na hatua
hiyo, Mawakili wa Serikali waliweka pingamizi za awali wakipinga Mahakama Kuu kusikiliza maombi ya dhamana yaliyowasilishwa na
mshitakiwa.
Katika maombi hayo
Lema kupitia Mawakili wake waliiomba Mahakama Kuu ifanye mapitio ya majalada ya
kesi za Jinai namba 440 na 441 ya Mwaka huu,ambako
anakabiliwa na makosa ya uchochezi dhidi ya Rais Dk. John Magufuli.
Mawakili hao wa Lema waliomba maombi hayo kutokana na Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Desderi Kamugisha aliyesoma uamuzi uliokuwa na kurasa 22 hivi karibuni, ambapo alisema Mahakama hiyo alisema inamwachia Lema kwa dhamana kwa masharti atakayopewa na mahakama hiyo.
Hata hivyo,kabla hajakamilisha uamuzi huo akiwa katika ukurasa wa 21
kati ya 22, Mawakili wa serikali walisimama na kudai Serikali inakusudia kukata rufaa juu ya uamuzi huo.
Baadhi ya wabunge waliofika mahakamani kwa ajili ya kufuatili kesi
hiyo ya Lema ni Mbunge wa Modnuli Julius Kalanga,Dk. Mollel(Siha) na
wabunge wa viti maalum Secilia Pareso(Karatu) na Joyce Mukya(Arusha
Mjini),wote kutoka Chadema
Nje ya mahakama hiyo ulinzi wa askari polisi na magereza uliendelea
kuimarishwa ambapo kulikuwa na askari wenye silaha za moto katika eneo
la viwanja vya mahakama hiyo pamoja na gari la maji ya kuwasha.
Mwisho

No comments:
Post a Comment