NA ELIYA MBONEA, ARUSHA
KESI za ugaidi zinazowakabili watuhumiwa wa matukio ya ugaidi katika
Jiji la Arusha zimeendelea kuahirishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha
kutokana na upelelezi kutokamilika.
Kesi hizo kwa sasa zimepangwa kutajwa siku moja ambapo ziliahirishwa
jana kwa nyakati tofauti na Mahakimu tofauti.
Akiahirisha kesi hizo mahakamani hapa Hakimu Mkazi Devotha Msofe alidai
kesi zilizokuwa kwake ambazo ni PI namba 52,53,55,56,57 na 60 zitatajwa tena
Novemba 21, Mwaka huu.
Uamuzi wa kuziahirisha kesi hizo ulitolewa baada ya upande wa
Mawakili wa Serikali wakiongozwa na Wakili Kombe kuomba tarehe nyingine ya
kutajwa kutokana na kutokamilisha upelelezi.
“Mheshimiwa Hakimu upande wa Serikali tunaomba tarehe nyingine ya
kutajwa kutokana na upelelezi kutokamilika,” alisema Wakili Kombe.
Kwa upande mwingine kesi nyingine za ugaidi zinazowahusu wakazi wa
mkoani Pwani wanaodaiwa kuwahifadhi watuhumiwa wa ugaidi ziliahirishwa kwa
Hakimu Mkazi Simon Bayo Hadi Novemba 21, Mwaka huu.
Naye Hakimu Mkazi Hawa Mguruta kwa upande wake aliahirisha kesi za
watuhumiwa hao hadi Novemba 21, Mwaka huu kutokana na upande wa Serikali kudai
kuwa unaendelea na upelelezi.
Mwisho.
namba Mahakami tofauti . WAKAZI watano wa wilaya ya
Rufiji mkoani Pwani wamepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kwa
madai ya kumhifadhi mtuhumiwa wa ugaidi aliyeuwa kwa kupigwa risasi na jeshi la
polisi Yahaya Hussein (31) ‘Sensei’.
Kupandishwa kizimbani kwa watuhumiwa hao watano kumefanya idadi ya
wanaodaiwa kumhifadhi marehemu Sensei na Mwenzake Mohamed Mnyele kufikia Saba
baada ya awali kupandishwa kizimbani watuhumiwa wawili.
Akiwasomea Hati ya Mashitaka upya watuhumiwa wote Saba, katika
kesi namba 74 ya Mwaka 2014 Wakili wa Serikali Felix Kwetukia alidai kuwa,
watuhumiwa wote walitenda kosa hilo Agosti 9, Mwaka huu.
Wakili Kwetukia mbele ya Hakimu Mkazi Simon Bayo alidai kwamba,
wakiwa maeneo ya Ikwiriri, wilayani Rufiji mkoani Pwani watuhumiwa hao
walimhifadhi gaidi Yahaya Hussein Sensei.
“Kosa la pili linalowajkabili nyote kwa pamoja ni la
kumhifadhi mtuhumiwa wa ugaidi Mohamed Mnyele,” alidai Wakili wa Serikali
Kwetukia.
Aliwataja watuhumiwa kwa pamoja katika kesi hiyo kuwa ni Sadick
Hussein, Masumai Kabora, Ismail Juma, Bahari Iddi, Lazaro Salum, Abdulah
Abubakar na Aman Issa.
Aidha Wakili wa Serikali Kwetukia alidai kwamba upelelezi wa kesi
hiyo pamoja na kesi namba 75 ya mtuhumiwa Shaban Idd anayedaiwa kuhifadhi pia
watuhumiwa wa ugaidi bado haujakamilika. Hivyo kesi hizo ziliahirishwa hadi
Novemba 7, Mwaka huu.
Katika hatua nyingine mahakamani hapo kesi zote zinazowahusu
watuhumiwa wa vitendo vya ugadi ikiwamo kukutwa na mabomu, kumwagia watu
tindikali, milipuko ya mabomu Mgahawa wa VAMA, Arusha Night Park, Viwanja vya
Soweto na Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph wa Mfanyakazi zimepangwa kusomwa
siku moja.
Kutokana na kupangwa kwa siku moja zote, iliwalazimu Mahakimu
watano kupishana kwa nyakati tofauti kwa ajili ya kuziahirisha kutokana na
upelelezi wake kutokukamilika, ambapo zote zimepangwa hadi Novemba 7, Mwaka
huu.
Mahakimu hao waliongozwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi Mustapha
Siyani aliyeahirisha kesi ya ugaidi namba 43, ambapo upande wa
Wakili wa Serikali alikuwa ni Lilian Mmasi.
Hata hivyo katika kesi hiyo yenye watuhumiwa 9, tayari mtuhumiwa
wa 4 Abdallah Maginga ndiye aliyewakilishwa na Wakili wa kujitegemea Zaharan
Kisilwa ambaye pia aliomba kupatiwa jalada la kesi hiyo kwa ajili ya kulisoma.
Hakimu Mkazi Devotha Msofe aliahirisha kesi Saba namba 44,
52,53,55,56,57,60, akifuatiwa na Hakimu Mkazi Hawa Mguruta kesi mbili namba 63
na 65. Alifuatiwa na Hakimu Mkazi Simon Bayo aliyeahirisha kesi mbili namba 74
na 75 na Hakimu Mkazi Rose Ngoka aliyeahirisha kesi moja.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment