Na JLA: Arusha
WATU wanne wamenurika kwenda jela miaka mitano baada ya kulipa faini ya Sh. Milioni Tano kila mmoja huku Serikali ikitaifisha gari lao aina ya Fuso namba T. 264 APV.
Akizungumza jijini hapa jana Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Arusha Daniel Naomba alisema watu hao wamekutwa na hatia ya kusafirsha kwa njia haramu raia 96 wa Ethiopia.
Alisema mbali na kuhukumiwa Mahakama iliamuru pia gari aina ya Fuso namba T. 264 APV kutaifishwa na Serikali kutokana na kutumika kuwasafirishia wahamiaji hao haramu.
Alisema kesi hiyo iliyokuwa ikisikilizwa katika Mahakama ya wi;aya ya Ngorongoro ilitolewa uamuzi Januari 2, Mwaka huu na kuwakuta na hatia watuhumiwa wote wanne.
“Watuhumiwa wote ni wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro wote kwa pamoja baada ya kutolewa hukumu walilipa faini ya Sh. Milioni tano kila mtuhumiwa,” alisema Naomba.
Kwa upande wa raia wa Ethiopia waliokutwa na hatia tayari wameanza kutumikia kifungo cha miaka mitano jela baada ya kushindwa kulipa fidia ya Sh. Milioni Tano.
Ofisa huyo wa Uhamiaji aliwataja Watanzania waliolipa faini kuwa ni Said Augustino Mrembe mmiliki wa Fuso, Taritoi Sarikoki Laizer msindikizaji, Romuald Clemence Tarimo na Samwuel Mwashingo madereva na Petro Gilayado Kisima utingo
Raia hao 96 wa Ethiopia walikamatwa Desemba mwaka jana wakiwa nchini kinyume cha sheria za nchi.
Wakati huo Ofisa huyo wa Uhamiaji amebainisha kuwa wahamiaji haramu 13 nao wamehukumiwa jela siku 14 baada ya kushindwa kulipa faini ya Sh. 50,000.
Alisema watuhumiwa hao walikamatwa katika eneo la Kisongo jijini Arusha, ambapo mwanamke aliyetajwa kuwapa hifadhi hao naye akinusurika kwenda jela baada ya kulipa faini ya Sh. 50,000
@@@@
No comments:
Post a Comment