Meneja afariki gafla akiwa maliwato ofisini
MENEJA wa Wakala wa Kituo cha Uchunguzi wa Magonjwa ya Mifugo Kanda ya Kaskazini Dk. Adam Tulingwa (56) amefariki gafla akiwa ndani ya choo cha ofisi.
Tukio la aina yake lililowashtua wakazi wa jiji la Arusha limetajwa kutokea juzi Saa 9.30 alasiri, ambapo Kamanda wa P[olisi Mkoa wa Arusha Liberatus Sabas amelithibitisha.
Taarifa kutoka eneo la tukio zilidai jana kwamba Dk. Tulingwa akiwa ofisini kwake aliondoka kwa ajili ya kwenda maliwatoni.
Hata hivyo baada ya juhudi nyingi za wafanyakazi kumtafuta kutokana na maelezo kuwa wateja walikuwa wakiendelea kumsubiria kwa ajili ya kupatiwa huduma.
“Baadhi ya watumishi walifika ofisini kwake wakakuta mlango upo wazi huku simu ikiwa mezani,” alidai mtoa taarifa.
Aliendelea kueleza kwamba hatua ya kutokuwapo ofisini ilionekana kuwashtua zaidi wafanyakazi waliokuwa wakimtafua.
Hata hivyo baada ya juhudi za kumtafuta maeneo tofauti ikiwamo maliwatoni ndipo walipoamua kuvunja mlango wa maliwato iliyokuwa imefungwa ndipo walimkuta akiwa amekwisha fariki.
Kwa upande wake Kamanda Sabas akizungumzia taarifa hiyo alisema kwamba jeshi hilo linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.
Dk. Tulingwa aliajiriwa Januari 5, Mwaka 1985 akiwa Daktari wa mifugo Daraja la II mara baada ya kumaliza Shahada ya Kwanza nay a Pili kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine Morogoro.
No comments:
Post a Comment