Tuesday, October 31, 2017

TANGAZO LA KUITWA KAZINI -TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali za kada za Afya walioomba kazi kuanzia tarehe 25/07/2017 hadi tarehe 30/08/2017 kuwa mchakato wa kuwapangia vituo vya kazi umekamilika.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS

Anuani ya Simu: “TAMISEMI”
Simu Na: (026) 2322848, 2321607
2322853, 2322420
Nukushi: (026) 2322116, 2322146
2321013
Barua pepe: ps@tamisemi.go.tz
Unapojibu tafadhali taja:
Tawala za MKOA na
Serikali za Mitaa,
Jengo la Mkapa,
2 Barabara ya hospitali,
S.L.P. 1923,
41185 DODOMA.
Kumb. Na. CD. 162/355/01
30 Oktoba, 2017

TANGAZO LA KUITWA KAZINI
OR TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto inapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi
mbalimbali za kada za Afya walioomba kazi kuanzia tarehe 25/07/2017 hadi
tarehe 30/08/2017 kuwa mchakato wa kuwapangia vituo vya kazi
umekamilika.

Aidha, mnatakiwa kuripoti katika vituo vya kazi mlivyopangiwa katika muda
wa siku kumi na nne (14) kuanzia tarehe ya tangazo hili mkiwa na vyeti halisi
(Originals Certificates) vya masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea
kwa ajili ya kuhakikiwa na mwajiri kabla ya kupewa barua ya ajira.

Orodha ya majina ya waliopangiwa vituo vya kazi inapatikana kupitia tovuti
ya OR TAMISEMI www.tamisemi.go.tz. Hakutakuwa na mabadiliko ya vituo,
watakaoshindwa kuripoti katika muda uliopangwa, nafasi zao zitajazwa na
waombaji wengine wa kada husika.

Kwa wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue
kuwa hawakupata nafasi hivyo wasisite kuomba kwa mara nyingine nafasi za
kazi zitakapotangazwa. Nafasi za Wauguzi na Wahudumu wa Afya
zitatangazwa mara baada ya kukamilisha zoezi la uchambuzi na uhakiki wa
vyeti.

Waajiri wote mnaelekezwa kuwapokea, kuhakiki vyeti na kuwafanyia
mafunzo elekezi (Induction Course) kabla ya kuwapangia vituo vya kazi.
Limetolewa na:-

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
OR – TAMISEMI
30/10/2017

No comments:

Post a Comment